Swali: Mmoja katika watu wanaowasomea watu anasema kuwa huomba msaada kutoka kwa majini waislamu kwa madai ya kwamba ana fatwa kuhusu hilo. Je, hili linajuzu?

Jibu: Kuhusiana na kwamba ana fatwa juu ya hilo mimi sijui mwanachuoni yeyote miongoni mwa wanachuoni vigogo – wenye kujifanya ni wanachuoni ni wengi – ama wanachuoni vigogo hawajuzishi hilo. Haijuzu kutaka msaada kutoka kwa majini. Ni kipi kimechokujulisha kuwa ni waislamu? Hata kama tutachukulia kuwa ni waislamu, ni ipi dalili ya kutaka msaada kutoka kwa watu wasioonekana na walioko kwenye ulimwengu mwingine usiouona?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-4-6.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020