Fajr kwa ambao wanaanza safari alfajiri mapema

Swali: Waalimu wa kike wanaofanya kazi nje ya ar-Riyaadh ambao wanatoka kabla ya swalah ya Fajr na wanafika katika masomo yao baada ya kuchomoza kwa jua. Je, waswali ndani ya gari au waswali vipi?

Jibu: Hili limekwishaulizwa na tumewajibu. Ni lazima kwao kuswali ndani ya gari. Vinginevyo wasimame. Wakiweza wanatakiwa kusimama na kushuka pale watapoweza kulisimamisha. Watashuka ili waswali kisha wapande tena. Tumewaandikia wahusika kubadilisha nidhamu hii. Wabadilishe nidhamu yao kwa njia ya kwamba safari ianze baada ya swalah. Tumewaandikia wahusika kuhusu hili na pengine wakaitikia – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23198/حكم-صلاة-الفجر-لمعلمات-يخرجن-مبكرا
  • Imechapishwa: 24/11/2023