Swali: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kuchukua elimu kutoka kwenye chaneli za Televisheni?

Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ametwambia:

فَاسْأَلُواْ أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لاَ تَعْلَمُونَ

“Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.” (16:43)

Tunatakiwa kuchukua elimu kutoka kwa wanachuoni na watu wenye ukumbusho. Elimu haichukuliwi kutoka kwenye chaneli. Ikiwa tunasema kuwa haifai kuchukua elimu kutoka kwenye kitabu peke yake, vipi tusemeje kuhusu kuchukua elimu kutoka kwenye chaneli ambapo ndani yake huingia mtu ni mtu wakiwemo wapotevu na wazuri? Elimu haitakiwi kuchukuliwa kutoka kwenye chaneli. Haziaminiki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls–14340420.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015