Uislamu una kundi moja – hauna makundi makundi

Swali: Kama jinsi mnavyojua kipindi cha mwisho kumetokea wanafunzi kugawanyika na kutawanyika katika makundi na vipote. Ni ipi nasaha yako?

Jibu: Haijuzu kugawanyika makundi na vipote. Waislamu ni kundi moja:

إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ

”Hakika huu Ummah wenu ni Ummah mmoja; Nami ni Mola wenu, basi niabuduni.” (21:92)

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

”Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Allaah kwenu, pale mlipokuwa maadui (kati yenu); kisha Akaunganisha nyoyo zenu, mkawa kwa neema Yake ndugu; na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto Akakuokoeni humo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni alama Zake mpate kuongoka. Na uweko (watokeze) kutoka kwenu Ummah unaolingania kheri na mema na unaokataza munkari. Na hao ndio waliofaulu. Na wala msiwe kama wale ambao walifarikiana na wakakhitilafiana baada ya kuwajia hoja bayana. Na hao watapata adhabu kuu.” (03:103-105)

وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ ۖ وَاصْبِرُوا

”… na wala msizozane, mtavunjikwa moyo, na itapotea nguvu yenu, na subirini. Hakika Allaah Yu Pamoja na wanaosubiri.” (08:46)

Kukitokea tofauti kurejelewe Qur-aan na Sunnah:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni (njia) bora na matokeo mazuri zaidi.” (04:59)

Tusibaki katika tofauti, migawanyiko na makundi makundi. Haya yamekatazwa na Dini na yanasababisha athari mbaya. Ni lazima Waislamu wawe na umoja, kufahamiana na kufuata njia moja ili Ummah uwe na haiba, ushirikiano na mapenzi. Kwa kuwa kugawanyika kunaleta migogoro. Bali huenda likapelekea mpaka katika kupigana:

وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِن بَعْدِهِم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ

Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana wale ambao (walikuja) baada yao, baada ya kuwajia hoja bayana.” (09:253)

Tofauti wakati mwingine inapelekea Waislamu kunyanyuliana silaha baina yao. Haijuzu kutofautiana.

Kuhusu kutofautiana katika masuala ya Fiqh ni jambo ambalo limetokea kwa kiasi cha Ijtihaad. Ama watu kutofautiana makundi makundi ni jambo ambalo halijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls–14340420.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015