Ibn ´Uthaymiyn kuhusu Jihaad Kashmir na Khawaarij wanaorudi

Swali: Je, Jihaad Kashmir ni sahihi?

Jibu: Jambo la kwanza Jihaad inahitajia uongozi wa Khaliyfah au kiongozi. Hilo halipatikani kwa leo.

Jambo la pili Jihaad inahitajia mtu atoke na aende aweze kufaidika na kutumia fursa. Ni jambo lenye kujulikana ya kwamba hilo halipatikani leo. Ndege zinashambulia kwa juu. Wale wote walioko chini ya ndege wanakuwa chini ya nguvu zao. Hakuna faida. Hapo mwanzoni vita vilikuwa katika ardhi. Watu walikuwa wakipigana kwa mikuki na panga. Matokeo yake kunapatikana faida.

Jambo la tatu wanaoshiriki katika vita hivi ni watu ambao wanataka kujifanya wawe huru kwa kuwa ni wenye kukandamizwa katika miji yao. Wanakuja ili kujifanya kuwa huru. Kisha baada ya hapo wanawapulizia wengine sumu na wanawadanya kuwachukia viongozi wao. Baada ya hapo wanarejea katika miji yao na chuki dhidi ya rai na watawala. Kwa hivyo kunatokea madhara makubwa. Sitaki kutoa mfano wao. Lakini zingatieni miji mingi. Mji ukiwa na usalama na vita vikafanikiwa na mlinganizi mmoja akataka kulingania kwa mujibu wa Manhaj na madhehebu yake – katika miji kuna mamlaka ya Dini rasmi ambayo hayamruhusu yeyote kuzungumzia kuhusu huyu ana madhehebu yanayokwenda kinyume na yule. Ina maana ya kwamba Da´wah sahihi haipatikani huko. Hili ni tatizo. Msimamo wetu kwa ndugu hawa tunamuomba Allaah Awape nusura na Awasaidie. Hili ndio tuliwezalo. Na kama tunaweza kusaidia kwa mali tunapigana vilevile Jihaad kwa mali.

Swali: Hapo mwanzoni ulisema kuwa inajuzu kwenda sehemu zingine.

Jibu: Mambo yanabadilika kutokana na natija. Wakati vita vilitokea Afghanistan tulisapoti hilo na kuwaambia watu waende huko. Lakini natija ikawa kinyume kabisa na tulivyotaraji. Wale wanaorejea kutoka huko wana hali ambazo zinajulikana. Isipokuwa wale waliosalimishwa na Allaah (´Azza wa Jalla). Mnajua wenyewe wale wanaobaki huko namna wanavyopigana wao kwa wao.

Swali: Tumepata khabari ya kwamba una Fatwa imeenea kati ya Mujaahiduun Kashmir inayosema kuwa unapendekeza Jihaad Kashmir na kwamba uongozi ni sahihi.

Jibu: Hapana, si kweli.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (207 B)
  • Marejeo: 1420-02-19/1999-06-03
  • Imechapishwa: 09/04/2015