Swali: Mwenye kufunga Sitta Shawwaal na ilihali yuko na deni la Ramadhaan. Je, Swawm yake ni sahihi?

Jibu: Kunatarajiwa kuwa ni sahihi lakini hata hivyo amekosea. Lililo la wajibu ni yeye atangulize kwanza faradhi na kulipa deni lililo juu yake la Ramadhaan mwanzoni wa Shawwaal kisha baada ya hapo ndio afunge Sitta Shawwaal. Kwa kuwa katika Hadiyth imekuja:

“Atakayefunga Ramadhaan na akaifuatisha na Sitta Shawwaal.”

Mwenye deni hakufunga Ramadhaan yote. Anachotakiwa ni kulipa kwanza madeni alonayo kisha ndio afunge Sitta katika masiku yatayokuwa yamebaki katika [mwezi wa] Shawwaal.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/%205841
  • Imechapishwa: 09/04/2015