Wakati mwezi huu mtukufu [wa Ramadhaan] unapoisha ni wajibu kwa Muislamu aogope matendo yake kurudishwa na kutokukubaliwa na amuombe Allaah ukubaliwaji na mwisho mwema na msamaha juu ya mapungufu. Wasidanganyike juu ya nafsi zao.

Wasikomeke juu ya mwezi huu peke yake na pindi unapoisha wanarejea katika ughafilikaji, uvivu na uzembe. Waendelee kumuabudu Allaah. Wanamuabudu Allaah na hawaabudu mwezi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anaabudiwa katika kila nyakati na kila hali na sio katika hali fulani tu, mwezi au wakati fulani. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ

“… na mwabudu Mola wako mpaka ikufikie yakini.” (15:99)

Bi maana mauti. Endelea na ´ibaadah mpaka wakati wa kufa. Muislamu hana likizo ya ´ibaadah. Anamuogopa Allaah, kumukhofu, anamuabudu na anamcha katika kila wakati na hali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/%205841
  • Imechapishwa: 09/04/2015