Duka kwa ajili ya kuuza nguo za kiume za kizungu

Swali: Je, inafaa kufungua duka kwa ajili ya kuuza nguo za kizungu na linatembelewa na asilimia kubwa ya vijana wanaotaka kusafiri kwenda katika miji ya uasherati na ukahaba?

Jibu: Ikiwa ni miongoni mwa mavazi yanayovaliwa na waislamu, hata kama yanatengenezwa nchi za nje kama vile London na USA. Lakini haifai endapo mavazi hayo ni kujifananisha na makafiri.

Swali: Kwa mfano suruwali na tai?

Jibu: Haijuzu ikiwa ni miongoni mwa mavazi ya makafiri na si katika mavazi ya waislamu. Asiwasaidie katika batili. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖوَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Saidianeni katika wema na kumcha Allaah na wala msishirikiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Swali: Ikiwa waislamu na makafiri wote wawili wanashirikiana katika kuyavaa?

Jibu: Ikiwa ni mavazi ya kushirikina, kama vile gari, sio kitu maalum mkwa makafiri. Vivyo hivyo ndege ni kitu cha kushirikiana na haina neno. Ndege sio za makafiri pekee. Vilevile magari sio za makafiri pekee.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22703/حكم-فتح-محل-لبيع-الملابس-الرجالية-الافرنجية
  • Imechapishwa: 31/07/2023