Swali: Swawm inasihi mtu akifungiwa na watoto kwa mfano yuko na watoto watano na kila mmoja anamfungia baba yao siku sita?

Jibu: Hapana vibaya. Anaweza kufungiwa na watoto, ndugu zake au watu wengine. Mmoja akafunga siku sita, mwingine akafunga siku kumi na tano na kadhalika.

Swali: Vipi ikiwa wote watamfungia katika siku moja?

Jibu: Udhahiri ni kwamba hakudhuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayekufa na anadaiwa swawm, basi atafungiwa na walii wake.”

Kila mmoja amefunga siku moja.

Swali: Je, wanapata dhambi wasipomlipia?

Jibu: Hapana, inapendeza. Kinachotambulika kati ya wanazuoni ni kwamba ni jambo limewekwa katika Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22709/حكم-صوم-اولاد-المتوفى-عنه-بتقسيمه-بينهم
  • Imechapishwa: 31/07/2023