Dini zote ni batili baada ya kuja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Dini ya kiyahudi ni batili. Dini ya kinaswara ni batili. Hazikubaliwi mbele ya Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” (03:85) 

Wanajitaabisha katika ´ibaadah zao ambazo wamezusha. Wanajitaabisha sana. Yote wayafanyayo ni kama upepo hautowafaa kitu. Hazitokubaliwa. Kauli Yake (Ta´ala):

وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“… naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”

Lau watashinda duniani hawatoshinda huko Aakhirah. Ni dini batili.

Wale manaswara ambao wanajinasibisha na ´Iysaa bin Maryam (´alayhas-Salaam) ni waongo. al-Masiyh hana lolote kuhusiana na wao. Lau angelikuja al-Masiyh angeliwapiga vita. Atashuka katika zama za mwisho na hatokubali isipokuwa Uislamu. Atavunja misalaba. Ataua nguruwe. Hatokubali watoe kodi. Hakuna dini atayokubali isipokuwa Uislamu tu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/349)
  • Imechapishwa: 08/05/2023