Salaf (Rahimahumu Allaah) wameusia kushikamana na Qur-aan na Sunnah. Abu Barzah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Allaah amekutajirisheni – amekuhuisheni – kwa Uislamu na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]

Abu ´Abdillaah amesema:

“Hapa imekuja kwa amekutajirisheni, lakini inatakiwa iwe amekuhuisheni.”

Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hutokosea njia muda wa kuwa unafuata mapokezi.”[2]

az-Zuhriy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wanazuoni wetu waliotangulia walikuwa wakisema: “Kushikamana na Sunnah ni uokozi.”[3]

Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Sunnah ni safina ya Nuuh; yule atakayeipanda basi ataokoka na yule atakayebaki nyuma basi atazama.”[4]

Shurayh na Ibn Siyriyn (Rahimahumaa Allaah) amesema:

“Hatutopotea muda wa kuwa tumeshikamana na mapokezi.”[5]

al-Awzaa´iy amesema:

“Tunazunguka na Sunnah kule inakozunguka.”[6]

´Abdullaah bin Mas´uud bin ´Utbah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hutokosa njia muda wa kuwa unafuata mapokezi.”[7]

´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) amesema:

“Lazimiana na Sunnah. Hakika kwa idhini ya Allaah ni kinga kwako.”[8]

[1] al-Bukhaariy.

[2] as-Sunnah, uk. 28, ya Muhammad bin Naswr.

[3]ad-Daarimiykatika ”as-Sunah”, al-Laalakaa’iyna al-Aajurriykatika ”ash-Shariy´ah”, uk. 314.

[4] al-Bayhaqiy.

[5] ar-Radd ´alaa al-Marriysiy, uk. 145, ya ad-Daarimiy.

[6] al-Laalakaa’iy (1/64).

[7]at-Twabaqaat (1/71) ya Ibn Abiy Ya´laa.

[8]Abu Daawuud (5/90), Ibn Wadhdhwaah katika ”al-Bid´a wan-Nahiy ´anhaa”, uk. 30, na Abu Nu´aym katika ”Hilyat-ul-Awliyaa’” (5/338).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 08/05/2023