Jaabir ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema wakati wa hijjah ya kuaga:

“Hakika mimi nimekuachieni yale ambayo hamtopotea baada yangu endapo mtashikamana nayo; Kitabu cha Allaah.”[1]

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kuna kanuni yenye manufaa inayobainishia ulazima wa kushikamana na Ujumbe, kwamba furaha na uongofu unapatikana kwa kumfata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba upotevu na maangamivu kunapatikana kwa kule kwenda kinyume naye. Kila kheri inayopatikana, ni mamoja iliyoenea au maalum, ni yenye kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na kwamba kila shari ulimwenguni itokayo kwa mja sababu yake ni kwenda kinyume na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kujahili yale aliyokuja nayo. Kufaulu kwa mja duniani na Aakhirah ni kwa kule kufuata Ujumbe wake.

Ujumbe ni kitu cha lazima kwa waja. Hawawezi kujitosheleza nao. Wanauhitajia zaidi kuliko wanavohitajia kila kitu. Ujumbe ni roho, nuru na uhai wa ulimwengu. Ni manufaa gani yana ulimwengu ukikosa roho, nuru na uhai? Dunia ni yenye giza na yenye kulaaniwa isipokuwa kile kilichochomozewa na nuru ya Ujumbe. Moyo wa mja ambaye haukuchomozewa na nuru ya Ujumbe na hakupata sehemu ya uhai na roho yake yuko kwenye giza na ni katika wafu. Allaah (Ta´ala) amesema:

أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا

“Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamuhuisha na tukamjaalia nuru anatembea kwayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yuko katika viza si mwenye kutoka humo?”[2]

Namna hii muumini alikuwa amekufa kwenye giza la ujinga ambapo Allaahakamuhuisha kwa roho ya Ujumbe na nuru ya imani na akamfanya kuwa na nuru akitembea kati ya watu. Allaah (Ta´ala) ameita Ujumbe Wake kuwa ni roho. Roho inapokosekana, basi unakosekana uhai. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ

”Na hivyo ndivyo tulivyokuletea Roho katika amri Yetu. Hukuwa unaelewa nini Kitabu na wala imani, lakini tumeijaalia kuwa ni nuru, tunamwongoza kwayo Tumtakaye kati ya waja Wetu. Na hakika wewe bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka.”[3]

 

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ

”Na hivyo ndivyo tulivyokuletea Roho katika amri Yetu. Hukuwa unaelewa nini Kitabu na wala imani, lakini tumeijaalia kuwa ni nuru, tunamwongoza kwayo Tumtakaye kati ya waja Wetu. Na hakika wewe bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka.”[4]

Ametaja hapa misingi miwili: roho na nuru. Roho ni uhai na nuru ni nuru…[5]

Mja anahitajia Ujumbe zaidi kuliko mgonjwa anavohitajia dawa. Kikubwa kinachoweza kutokea wakati wa kukosekana dawa ni kufa kwa mwili. Lakini mja asipoipata nuru na uhai wa Ujumbe basi moyo wake unakuwa kifo ambacho hautarajiwi tena kuwa hai au kufurahi. Kwa hivyo hakuna kufaulu isipokuwa kwa kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah amewafanya kufaulu wale wenye kumfuata na kumnusuru (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yao. Amesema (Ta´ala):

فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Basi wale waliomuamini na wakamtukuza na wakamnusuru na wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu.”[6]

Hakuna waliowafaulu wengine wasiokuwa wao:

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu. Hao ndio waliofaulu.”[7]

Amewafanya maalum watu hawa kufaulu. Ni kama ambavo amewatunuku uongofu na kufaulu wale wenye kumcha ambao wanaamini yaliyofichikana, wanasimamisha swalah, wanatoa sehemu ya vile alivyowaruzuku, wanaamini yale yaliyoteremshwa kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale yaliyoteremshwa kabla yake na wana yakini juu ya Aakhirah. Hilo linathibitisha kuwa kuwepo na kutokuwepo kwa uongofu na mafanikio kunazungukia katika Ujumbe.”[8]

[1] Muslim (1218).

[2] 6:122

[3] 42:52

[4] 42:52

[5]Majmuu´-ul-Fataawaa (19/93-94).

[6] 7:157

[7] 3:104

[8]Majmuu´-ul-Fataawaa (19/97).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 22-24
  • Imechapishwa: 08/05/2023