Bid´ah ni kumkadhibisha Allaah na kumtukana Mtume

Katika kushuhudia kwako ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah ni lazima kumfuata katika Shari´ah yake na Sunnah zake. Usizushe katika dini yasiyokuwemo. Kwa ajili hii tunasema wale watu wa Bid´ah ambao wamezusha katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yasiyokuwemo hawakuhakikisha ushuhudiaji ya kuwa Muhammad ni Mtume wa Allaah. Haijalishi kitu hata kama watasema kuwa wanampenda na wanamuadhimisha. Lau wangelimpenda kikamilifu na kumuadhisha kikamilifu, basi wasingelimtangulia na kuingiza katika Shari´ah yake yasiyokuwemo.

Uhakika wa mambo ni kwamba Bid´ah ni kumtukana Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni kana kwamba mzushi huyu anasema kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakukamilisha dini wala Shari´ah.

Madhara mengine yanayopatikana katika Bid´ah, na ni madhara makubwa sana, ndani yake kuna kuikadhibisha maneno ya Allaah (Ta´ala):

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ

“Leo Nimekukamilishieni dini yenu.” (05:03)

Ikiwa Allaah (Ta´ala) ameikamilisha dini ina maana ya kwamba hakuna dini nyingine baada ya aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Watu hawa ni watu wa Bid´ah. Wamezusha katika dini yasiyokuwemo.

Vilevile wanamtukana Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kumtuhumu kuwa hakukamilisha Shari´ah kwa wanaadamu. Ni jambo lisilowezekana kwake kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/351-352 )
  • Imechapishwa: 08/05/2023