Dhikr hii ni yenye kuenea katika kila wakati?

Swali: Hadiyth ya Juwayriyah inayosema:

سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه، وَرِضـا نَفْسِـه، وَزِنَـةَ عَـرْشِـه، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu yote na himdi zote njema ni Zake kwa idadi ya viumbe Wake, radhi Yake, uzito wa ´Arshi Yake na wino wa maneno Yake.”[1]

Inasomwa asubuhi na jioni?

Jibu: Katika kila wakati. Inasemwa katika kila wakati na popote unapokuwa.

Swali: Dhikr hii inaweza kutumiwa kama kipimo juu ya aina zingine za Adhkaar kwa mfano kusema:

لا إله إلا الله عدد خلقه

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah kwa idadi ya viumbe Wake.”

الحمد لله عدد خلقه

“Himdi zote njema anastahiki Allaah kwa idadi ya viumbe Wake.”

au ni jambo maalum kwa Dhikr iliyotajwa hapo juu?

Jibu: Ni yenye kuenea. Hapana vibaya.

Swali: Vipi ikiwa mtu atasema:

لا إله إلا الله عدد خلقه رضا نفسه زنة عرشه

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah kwa idadi ya viumbe Wake, radhi Yake, uzito wa ´Arshi Yake?”

Jibu: Hapana neno.

[1] Muslim (04/2090).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23072/هل-الذكر-بلفظ-عدد-خلقه-عام-لكل-وقت
  • Imechapishwa: 26/10/2023