Bi harusi hakutamka wazi kuridhia kwake

Swali: Nimemuoa binamu yangu na baba yake ndiye amesimamia suala la kumuozesha ambapo mjomba na kaka yake ndio walikuwa mashahidi. Msichana aliridhia kwa moyo msafi, lakini hawakumshauri kabla ya ndoa kumsikia kama ameridhia.

Jibu: Hapana, akiingia kwake hali ya kuridhia basi ameridhia. Alipoingia nyumbani kwake na akanyamaza ina maana kuwa ameridhia.

Swali: Kwa hiyo ndoa ni sahihi?

Jibu: Haina neno kabisa. Ondoa wasiwasi wa shaytwaan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23076/هل-يصح-عقد-من-لم-تصرح-برضاها
  • Imechapishwa: 26/10/2023