Swali 60: Ni vita vipi vilivyotokea mwaka wa nane?

Jibu: Katika mwezi wa Jumaadaa al-Uulaa, vita vya Mu’tah vilifanyika ambapo Zayd bin Harithah, Ja’far bin Abiy Twaalib na ´Abdullaah bin Rawaahah (Radhiya Allaahu ´anhum) waliuwawa hali ya kuwa ni mashahidi.

Katika mwaka huohuo Ramadhaan kulifanyika Ushindi Mkubwa. Sababu ya vita hivyo ilikuwa kwamba Quraysh walivunja makubaliano yao ya kuwasaidia Banuu Bakr juu ya kumuua Khuza’ah kwenye Haram. Huo ni Ushindi ambao Allaah aliutia nguvu Uislamu na yakavunjwa masanamu. Kisha baada ya hapo kukafuatia vita vya Hawaazin.

Mwaka huo pia kulitokea vita vya Hunayn na kisha kuzingirwa kwa Twaaif. Mji huo haukufunguliwa mpaka mwaka uliofuatia wakati ambapo wakazi waliingia ndani ya Uislamu. Wakiti alipokuwa njiani akirejea nyumbani na baada ya kugawanya ngawira za vita katika Dhul-Qa’dah Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akaamua kuingia katika ‘Umrah kutokea Ji’irraanah.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 124
  • Imechapishwa: 26/10/2023