Dereva wa basi la wanafunzi na swalah ya mkusanyiko

Swali: Bwana mmoja anafanya kazi kama dereva wa kuwaendesha wanafunzi. Baada ya wanafunzi kutoka na basi, anakosa swalah ya mkusanyiko ya Dhuhr msikitini. Akiswali mkusanyiko, anachelewa sana kazini, jambo ambalo linaweza kumletea matatizo. Je, inafaa kwake kuswali peke yake?

Jibu: Ndio. Huyu anapewa udhuru, kwa kuwa yuko kazini. Akiacha kazi hii kazi inaharibika. Analipwa mshahara kwa ajili ya kazi hiyo na ameaminiwa. Acheleweshe swalah muda wa kuwa anaswali ndani ya wakati wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 10/01/2024