Dalili ya kuangalia mahali pa kusujudia

Swali: Kuna Hadiyth Swahiyh kuhusu kuangalia pale mahali mtu anaposujudu?

Jibu: Sikumbuki isipokuwa yale makatazo yanayokataza kunyanyua macho juu. Kumepokelewa matahadharisho ya kunyanyua macho juu.

Swali: Ni ipi Sunnah?

Jibu: Wajibu ni kuteremsha macho. Makatazo ya kunyanyua macho juu kunatoa faida kwamba ni lazima kuteremsha macho chini.

Swali: Vipi kuhusu kumtazama imamu?

Jibu: Sunnah ni pale mahali unaposujudia. Kwa sababu ndio jambo lililo karibu zaidi na unyenyekevu.

Swali: Kumepokelewa kitu kinacholengesha mahali pa kutazama wakati mtu anaswali kwa kuashiria na wakati wa Tashahhud?

Jibu: Sikumbuki kitu juu ya hayo. Muhimu ajitahidi ambacho kiko karibu zaidi na kumletea unyenyekevu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22379/ما-دليل-النظر-الى-مكان-السجود-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 25/02/2023