Dalili wapi ndani ya Qur-aan kwamba sigara ni haramu?

Swali: Wako watenda madhambi wanasema kwamba hakuna dalili ya wazi kutoka ndani ya Qur-aan inayoharamisha sigara.

Jibu: Mwambie kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameharamisha vibaya. Je, kitu hicho ni katika vitu vizuri au vibaya?

يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ

“Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: “Mmehalalishiwa vilivyo vizuri.”[1]

Amesema alipokuwa akimsifu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ

“Anawahalalishia vilivyo vizuri na anawaharamishia vichafu.”[2]

Isitoshe madaktari wamekubaliana na watu wakakubaliana kuwa madhara yake ni makubwa, kwamba inasababisha madhara mengi na shari nyingi. Kuna watu wengi wanaokufa kwa sababu ya sigara. Madhara haya yanatubainishia ubaya wake. Hata hivyo matamanio humfanya mtu akawa kipofu.

[1] 05:04

[2] 07:157

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21990/ما-الدليل-على-تحريم-الدخان
  • Imechapishwa: 11/10/2022