Swali: Kuamrisha mema na kukataza maovu kunaingia katika aina za kulingania kwa Allaah?

Jibu: Hapana shaka kwamba miongoni mwa kulingania kwa Allaah ni kuamrisha mema na kukemea maovu. Ameliegemeza hilo katika maneno Yake (Jalla wa ´Alaa):

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu. Hao ndio waliofaulu.”[1]

Huku ni katika kuegemeza kitu maalum juu ya kilichoenea. Ambaye analingania kwa Allaah, anaamrisha mema au anakataza maovu kisha matendo yake yakaenda kinyume na yale anayolingania kwayo anaingia katika makemeo haya.

[1] 03:104

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21991/هل-الامر-بالمعروف-من-الدعوة-الى-الله
  • Imechapishwa: 11/10/2022