14. Maana na hukumu ya kurudisha nyuma na kupindisha maana

Maana ya kurudisha nyuma (الرد), kupindisha maana (التأويل), kushabihisha (التشبيه) na kufananisha (التمثيل) na hukumu ya kila kimoja katika hivyo

Kurudisha nyuma ni kule kukadhibisha na kupinga. Ni kama mtu kusema kwamba Allaah hana mkono wa kikweli wala wa kimafumbo, jambo ambalo ni ukafiri. Kwa sababu ni kumkadhibisha Allaah na Mtume Wake.

Kupindisha maana ni kule kufasiri. Makusudio hapa ni kuyafasiri maandiko kuhusu sifa za Allaah kinyume na vile alivyokusudia Allaah na Mtume Wake na kinyume na vile walivyofasiri Maswahabah na wale waliowafuata kwa wema.

Kuna kupindisha maana kwa sampuli tatu:

1 – Liwe limetokana na ijtihaad na nia njema kwa njia ya kwamba akibainikiwa na haki basi atajirudi kutokana na tafsiri yake mbovu. Huyu ni mwenye kusamehewa. Huu ndio mwisho wa uwezo wake. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[1]

2 – Liwe limetokana na matamanio na ushabiki na ana mashiko fulani katika lugha ya kiarabu. Ni dhambi nzito na sio ukafiri. Isipokuwa ikiwa kumekusanya kumtia kasoro Allaah. Katika hali hiyo itakuwa ukafiri.

3 – Lime limetokana na matamanio na ushabiki na hana mashiko yoyote katika lugha ya kiarabu. Huu ni ukafiri. Kwa sababu uhakika wake ni kukadhibisha kwa sababu hana mashiko yoyote.

[1] 02:286

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 11/10/2022