13. Hakuna andiko lolote litakuwa tatizo kwa Ummah mzima

Ufupisho wa maneno katika maandiko kwa upande wa uwazi na kutatiza

Jambo la uwazi na kutatiza kwa maandiko ya Shari´ah ni jambo linategemea na ambalo watu wanatofautiana kutegemea na elimu na ufahamu. Kitu kinaweza kuwa tatizo kwa mtu na kitu hichohicho kikawa kiko wazi kwa mtu mwingine. Kilicho cha wajibu wakati andiko ni lenye kutatiza ni kufuata yale yaliyokwishatangulia ambapo mtu anatakiwa kuacha kuingia sana kwa undani na kuchanganya maana yake. Kuhusu hali halisi ya maandiko ya Shari´ah ndani yake hakuna ambacho ni chenye kutatiza kwa njia ya kwamba hakuna mtu yeyote anayejua maana yake katika yale yanayowahusu katika mambo ya dini na dunia yao. Kwa sababu Allaah ameisifu Qur-aan kuwa ni nuru iliyo wazi na ubainifu kwa watu na kipambanuo na kwamba ameiteremsha hali ya kuwa ni yenye kubainisha kila kitu na kwamba ni uongofu na rehema. Hiyo inapelekea kwamba hakuna katika maandiko kitu ambacho kitakuwa tatizo kutegemea na hali kwa njia ya kwamba hakuna yeyote katika Ummah anayeweza kujua maana yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 33
  • Imechapishwa: 11/10/2022