Daima Qunuut katika Fajr

Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma Qunuut katika swalah ya Subh siku zote?

Jibu: Kufanya Qunuut katika Fajr ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Isipokuwa katika hali ya maafa kama vile kuingiliwa na ugonjwa wa mlipuko, adui kuzingira mji au kuwashambulia kwake waislamu. Katika hali kama hii imesuniwa kufanya Qunuut katika swalah ya Fajr na nyinginezo. Hivo ndivo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivofanya.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (15391)
  • Imechapishwa: 26/05/2022