Ni ipi hukumu ya kusafiri siku 40 na Jamaa´at-ut-Tabliygh

Swali: Ni ipi hukumu ya kutoka na Jamaa´at-ut-Tabliygh na kusafiri siku arobaini?

Jibu: Tumetaja mwanzoni kwamba ni lazima kwa muislamu kufuata mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake ikiwa kama kweli anataka kufaulu. Kuhusu yale yanayokwenda kinyume na mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi unatakiwa kuyatupilia mbali na kuyakataa. Kwa sababu ni mambo mepya na yaliyozuliwa.

Yule anayepita juu ya mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake, basi ongozana naye. Yule anayefuata mfumo uliyozuliwa unaotofautiana na mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake, basi unatakiwa kujiepusha ni mamoja ni Jamaa´at-ut-Tabliygh au mtu mwingine. Mfumo uko wazi. Mfumo wetu uko wazi na hatupakani mafuta nyuma juu yake:

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Kwamba hii ni njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate njia za vichochoro nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo alivyokuusieni kwayo mpate kumcha.”[1]

Kila kunapozuka kundi basi tunaondoka nalo na kuacha mfumo salama? Hiki ni kitu kisichojuzu.

[1] 6:153

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Manhaj-ul-Istiqaamah wal-Wasatwiyyah
  • Imechapishwa: 26/05/2022