Bwana harusi kukataza picha katika harusi yake

Swali: Ndoa yangu inakaribia – Allaah akitaka – na mimi ni miongoni mwa wale wanaoonelea picha za simu kuwa ni haramu. Hakika unajua kuenea kwa picha katika sherehe mbalimbali. Je, ni lazima kwangu kuwakataza wakati wataposimama kunipiga picha?

Jibu: Wawekee sharti ya kwamba wasifanye kitu hichi. Wawekee sharti hii. Endapo utaweza kuwakataza wakataze. Lakini wawekee sharti ya kwamba kusiwepo mambo ya picha wala kitu chochote cha maasi. Ukiweza kuwakataza kwa matendo ni wajibu kwako kufanya hivi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (48) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-5-26.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020