Swali: Wakati mwingine mtu anahisi uzito kuanza kusalimia kutokana na wingi wa wafanyakazi wa kikafiri.
Jibu: Wewe hukusikia nini alichosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa ni kitendo gani bora ambapo akajibu:
“Kulisha chakula na kumtolea salamu unayemjua na usimyemjua.”
Swali: Kuenea kwa dalili za salamu kunafahamisha ulazima wa kufanya hivo?
Jibu: Kuenea salamu ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Mtu akianza ndio bora zaidi. Ukianza kutolewa basi ni lazima uitikie. Muumini anakimbia mambo ya kheri ingawa kuanza kutoa sio lazima hata hivyo anatakiwa kuharakia kuanza. Ni kama mfano wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa:
“Ee Mtume wa Allaah! Ni Uislamu gani bora?” Akajibu: “Kulisha chakula na kumtolea salamu unayemjua na usimyemjua.”
Bora kwa mtu ni kuyakimbilia matendo mema.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22624/ما-حكم-السلام-على-جمع-فيهم-غير-مسلمين
- Imechapishwa: 09/07/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Msalimie yule unayekutana naye
Swali: Wakati fulani mtu anapita karibu na mnaswara au myahudi au ambaye hajui hali yake. Je, ampe salamu? Jibu: Amsalimie yule atayekutana naye. Kama ambavo amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kuulizwa: “Ni Uislamu ipi bora?” Akasema: “Kulisha chakula na kumtolea salamu unayemjua na usiyemjua.” Isipokuwa ukijua…
In "Salamu"
24. Ibn Baaz kuhusu kusalimiana baada ya swalah
Swali 24: Ni ipi hukumu ya salamu baada ya Sunnah[1]? Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa wenye kukutana katika safu mmoja akamsalimia mwengine na wakapeana mikono. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Hakuna waislamu wawili wanaokutana ambapo wakapeana mikono isipokuwa Allaah huwasamehe kabla hawajaachana.”[2] Anas (Radhiya Allaahu ´anh)…
In "Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah - Ibn Baaz"
108. Kueneza salamu
224- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Hamtoingia Peponi mpaka muamini na wala hamtoamini mpkaa mpendane. Je, nisikujulisheni jambo ambalo mtakapolifanya mtapendana? Enezeni salamu kati yenu.”[1] 225- “Mambo matatu atayeyakusanya basi atakuwa amekusanya imani; inswafu ya nafsi yako, kutoa salamu kwa watu wote na mtu kujitolea ingawa riziki imebana…
In "Huswn-ul-Muslim"