Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أبي إسحاق سعد بن أبى وقاص بن أهيب بن عبد مناف ابن زهرة بن كلاب النبي صلي الله عليه وسلم مرة بن كعب بن لوي القرشي الزهري رضي الله عنه، أحد العشرة المشهود لهم بالجنة، رضي الله عنهم، قال: ((جاءني رسول الله صلي الله عليه وسلم عام حجة الوداع من وجع اشتد بين فقلت: يا رسول الله إني قد بلغ بي من الوجع ما تري، وأنا ذو مال ولا يرثني إلا ابنة لي، أفاتصدق بثلثي مالي؟ قال: لا، قلت: فالشطر يا رسول الله؟ قال: لا قلت: فالثلث يا رسول الله، قال: الثلث والثلث كثير – أو كبير- إنك أن تذر ورثتك أغنياء خير من أن تذرهم عالة يتكففون الناس، وإنك لن تنفق نفقة تلتغي بها وجه الله إلا أجرت عليها، حتى ما تجعل في في أمراتكزقال: فقلت: يا رسول الله اخلف بعد أصحابي، قال: إنك لن تخلف فتعمل عملاً تبنغي به وجه الله؛ إلا أزدت به درجة ورفعة، ولعلك أن تخلف حتى ينتفع بك أقوام ويضر بك آخرون. اللهم أمص لأصحابي هجرتهم، ولا تزدهم على أعقابهم، لكن البائس سعد بن خولة)) يرثي له رسول الله صلي الله عليه وسلم أن مات بمكة. (متفق عليه)

6 – Abu Ishaaq Sa’d bin Abi Waqqaas Maalik bin Uhayb bin ‘Abdil-Manaaf bin Zuhrah bin Kilaab bin Murrah bin Ka’b bin Lu´ayy al-Qurashiy az-Zuhriy (Radhiya Allaahu ‘anh) – ambaye ni mmoja kati ya wale kumi waliobashiriwa Pepo – amesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwaka wa hajj ya kuaga alinijia kutokana na ugonjwa ambao uliokuwa umenishika kwelikweli. Nikamwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Ugonjwa umenifikisha kama unavyoniona, nami ni mwenye mali nyingi na wala hakuna atakayenirithi isipokuwa msichana wangu. Je, nizitoe swadaqah theluthi mbili za mali yangu?” Akajibu: “Hapana.” Nikasema: “Basi nitoe nusu yake, ee Mtume wa Allaah?” Akajibu: “Hapana.” Nikasema: “Je, theluthi?” Akajibu: “Theluthi [ni sawa toa] – na hiyo theluthi ni nyingi. Hakika kitendo cha kuwaacha warithi wako ni matajiri ni bora kuliko kuwaacha mafukara wakiomba watu. Hakika hutatoa matumizi yoyote hali ya kuwa unataka uso wa Allaah isipokuwa utapewa ujira kwayo. Hata kile unachokitia mdomoni mwa mke wako.” Nikamuuliza: “Ee Mtume wa Allaah! Nitaachwa baada ya wenzangu?” Akasema: “Hakika hutoachwa nyuma ukafanya kitendo kwa ajili ya kutafuta kwacho uso wa Allaah ispokuwa utazidi kwacho daraja na utukufu. Huenda ukaachwa nyuma mpaka watu wanufaike kwa sababu yako na wengine wadhuriwe kwa sababu yako. Ee Allaah! Wakamilishie Maswahabah wangu hijrah yao na wala usiwarejeshe nyuma kwa visigino vyao. Lakini masikini ni Sa’d bin Khawlah!” Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akamsikitikia kwa sababu alikufa Makkah[1]

Miongoni mwa faida za Hadiyth hii ni kwamba ikiwa mali ya mtu ni ndogo na warithi wake ni mafukara, bora zaidi asiache anatoa wasia wa chochote. Asiusie kitu kidogo wala kikubwa. Kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kule kuwaacha warithi wako hali ya kuwa ni matajiri ni bora kuliko kuwaacha hali ya kuwa ni wenye kuombaomba.”

Hili ni tofauti na wanavyodhania baadhi ya watu wajinga kuwa ni lazima kwa mtu kuacha anausia. Hili ni kosa. Mtu ambaye hali yake ni ndogo na warithi wake ni mafukara na hawana mali, haitakikani kwake kuusia. Bora ni kutousia.

Baadhi ya watu wa kawaida wengine wanafikiria kuwa ikiwa hakuacha anausia hapati ujira. Sivyo hivyo. Bali akiwaachia warithi wake mali anapewa ujira kwa hilo hata kama warithi watarithi kwa hali yoyote. Lakini ikiwa atachukua uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

“Kule kuwaacha warithi wako hali ya kuwa ni matajiri ni bora kuliko kuwaacha hali ya kuwa ni wenye kuombaomba.”

ujira wake katika hilo ni bora zaidi kuliko kutoa swadaqah ya kitu katika mali yake.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/57-58)
  • Imechapishwa: 24/01/2023