Bora Adhkaar zifanywe kwa mkono wa kulia II

Swali: Kuna kijana mmoja ametuswalisha na baada ya kumaliza kuswali akawa analeta Adhkaar kwa mkono wake wa kuume peke yake. Baadhi ya waswaliji wakashangazwa na wakamuuliza kijana yule ambapo akasema kuwa hiyo ndio Sunnah. Tunaomba utupe faida juu ya usahihi wa hilo?

Jibu: Alilofanya imamu ndio la sawa. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa alikuwa akihesabu Dhikr kwa mkono wake wa kuume. Ambaye ataleta Dhikr kwa mikono yote miwili ni sawa kutokana Hadiyth nyingi kuja kwa njia ya kuachia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/186)
  • Imechapishwa: 30/10/2021