Swali: Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema kuwa haifai kuuza vitu visivyokuwa na maana na akaleta mfano wa wadudu. Je, inafaa kuuza nzige au zimebaguliwa?

Jibu: Nzige zinaliwa:

”Tumehalalishiwa maiti aina mbili na damu aina mbili. Ama maiti mbili ni samaki na nzige, na ama damu mbili  ni bandama na ini.”[1]

Ikiwa haijuzu kufanya biashara ya nzige basi haijuzu pia kufanya biashara ya samaki. Inafaa kufanya biashara ya nzige kwa sababu ni zenye kuliwa na ni katika vitu halali.

[1] Ahmad (5690) na Ibn Maajah (3314).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 17/04/2021