Kuuza bidhaa za haramu katika nchi za kikafiri

Swali: Je, inafaa kwa muislamu katika nchi ya kikafiri kuuza bidhaa za haramu…?

Jibu: Hapana. Muislamu hauzi bidhaa za haramu, pasi na kujali maeneo alipo. Kwa sababu Allaah pindi anapoharamisha kitu basi huharamisha vilevile thamani yake. Wakati Allaah alipowaharamishia mayahudi kuuza shahamu za nyamafu, basi siagi hiyo waliiyeyusha kuwa mafuta na wakasema kuwa hawakuuza shahamu ili kuepuka makatazo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Haijuzu kufanya hivo. Jina halibadilishi uhalisia wa mambo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 17/04/2021