Baba wa wanaadamu, baba wa majini na baba wa Malaika

Swali: Swali hili limetoka Ufaransa linalosema: tunajua kuwa baba wa wanaadamu ni Aadam. Ni yupi baba wa Malaika na baba wa majini? Ni muumini yupi bora; muumini wa kibinaadamu au muumini wa kijini?

Jibu: Simjui ni nani baba wa Malaika. Ni nani alokwambia kuwa Malaika wana baba? Hili ni jambo ambalo halikuthibiti katika Qur-aan wala Sunnah. Usiulize juu ya hili kwa kuwa huku ni kujikalifisha ambako Allaah Hakuteremsha dalili yoyote juu yake.

Ama kuhusu baba wa majini ni Ibliys. Baba wa wanaadamu ni Aadam (´alayhis-Salaam).

Kuhusiana na muumini yupi ambaye ni bora kati ya wanaadamu na majini, Allaah ndiye Anajua zaidi. Tofauti iliopo ni: ni nani bora kati ya muumini wa kibinaadamu na Malaika? Hili ndio lina tofauti. Ama kuhusu muumini wa kijini na wa kibinaadamu, sijui.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-21.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020