Baba anamkataza kutangamana na marafiki wema

Swali: Mimi ni mwanafunzi katika shule ya sekondari na nimechagua marafiki wema. Lakini baba yangu ananizuia kutembea na kutangamana nao. Amenambia kwamba ataninunulia gari na nifanye nitakacho kukiwemo kuvuta sigara na mengineyo lakini nisitembee na watu hawa. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika si venginevyo utiifu unakuwa katika mema. Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

Hakuna kumtii baba, mtawala, kiongozi, mume, mke wala mtu mwingine katika yanayoenda kinyume na Shari´ah. Suhubiana na wema na tengeneza tabia yako na baba yako. Zungumza naye kwa upole na njia nzuri. Mtake udhuru na uzungumze naye kwa njia nzuri na mkinaishe kuwa watu hao ni ndugu zako kwa ajili ya Allaah, twakumbushana, twafaidishana na natumia baadhi ya wakati wangu katika kutangamana nao. Mweleze kuwa jambo hilo linakunufaisha katika dini yako na unataraji kwamba hatokukataza kutokana na jambo hilo. Fanya yote mawili na uendelee kumpa baba yako udhuru, kuzungumza naye maneno mazuri, kutangamana na kukumbushana na marafiki zako wema. Kusanya kati ya mambo mawili. Usiwe mjeuri wala mtovu wa adabu kwa baba yako. Kuwa mpole, mlaini, mwenye maadili mema kwa baba yako na maneno mazuri. Allaah (Subhaanah) amesema juu ya wazazi wawili ambao ni makafiri:

 وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ

“Hata hivyo suhubiana nao kwa wema duniani na ifuate njia ya anayerudi Kwangu.” (31:15)

Unalazimika kutangamana naye kwa wema. Hata hivyo usimtii katika yanayokudhuru na katika mambo yanayokwenda kinyume na Shari´ah ya Allaah (Subhaanah).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4063/ما-يفعل-من-يمنعه-ابوه-من-الرفقة-الصالحة
  • Imechapishwa: 06/06/2022