Baadhi ya Adhkaar za kukukinga na kijicho

Swali: Siku hizi kumeenea maradhi ya kijicho na wao wanajifakhari kwayo. Maradhi hayo yanawapata baadhi ya watu. Ni kipi unachowanasihi watu hawa?

Jibu: Ni lazima kutahadhari na kule mtu kukusudia. Ikiwa anakusudia kijicho basi analazimika kutahadhari jambo hilo. Ikijulikana kwamba anakusudia kitu hicho basi anapaswa kuchukuliwa hatua na kuadhibiwa. Lakini ikiwa sio kwa kutaka kwake basi hakuna anachoweza kufanya. Allaah haikalifishi nafsi isipokuwa vile inavyoweza.

Muislamu anasema asubuhi na jioni:

أعوذ بكلمات الله التامَّات من شرِّ ما خلق

“Najilinda kwa maneno ya Allaah yaliyo kamilifu kutokana na shari ya Aliyoyaumba.”

mara tatu.

Vilevile asome Aayaat-ul-Kursiy baada ya kila swalah:

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ

”Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye, Aliyehai daima, Mwenye kusimamia kila kitu.” (02:255)

Pia asome:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ

“Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee.” (112:01)

Kadhalika asome “al-Ikhlaasw” na “al-Falaq” mara tatu asubuhi na jioni na atoe salamu. Hakitomdhuru kijicho wala kitu kingine. Hiyo ni kinga ya kila kitu kibaya. Asome Aayaat-ul-Kursiy baada ya kila swalah na wakati wa kulala. Ndani yake mna kinga ya kila kitu kibaya.

Yote haya ni miongoni mwa sababu za kinga. Pia aseme:

أعوذ بكلمات الله التامَّات من شرِّ ما خلق

“Najilinda kwa maneno ya Allaah yaliyo kamilifu kutokana na shari ya Aliyoyaumba.”

mara tatu usiku na mchana. Au aseme:

بسم الله الذي لا يضرُّ مع اسمه شيءٌ في الأرض ولا في السماء، وهو السميع العليم

“Kwa jina la Allaah ambaye hakidhuru kwa jina Lake chochote mbinguni na ardhini Naye ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote.”

mara tatu usiku na mchana. Hii pia ni miongoni mwa sababu za kinga. Vivyo hivyo asome Aayah mbili za mwisho za Suurah al-Baqarah kila usiku:

آمَنَ الرَّسُولُ

“Mtume ameamini… ” (02:285)

Hii pia ni miongoni mwa sababu za ulinzi dhidi ya kila kitu kibaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4289/ما-حكم-من-كان-زوجها-لا-يصلي
  • Imechapishwa: 06/06/2022