28. Hivi ndivo wanavoamini Khashabiyyah

Khashabiyyah. ´Aqiydah yao ni moja kama Zaydiyyah na Shiy´ah. Kutokana na wanavodai wanawapenda watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zaidi kuliko wanavofanya wengine. Ni waongo. Ukweli wa mambo ni kwamba wao ni wenye kuwachukia watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zaidi kuliko wanavofanya wengine. Hakika si venginevyo wafuasi (شيعة) wa kweli wa watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wale wenye kumcha Allaah Ahl-us-Sunnah wal-Athar, pasi na kujali ni kina nani na wapi walipo. Ambao wanawapenda watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wote wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawamtaji yeyote miongoni mwao kwa mabaya. Hawamkosoi Swahabah yeyote. Ambaye atamtaja yeyote miongoni mwa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa njia mbaya, au akamkosoa yeyote miongoni mwao, au akajitenga mbali na yeyote miongoni mwao, au akamtukana yeyote miongoni mwao, au akamponda yeyote miongoni mwao, basi huyo ni Raafidhwiy, mwenye kwenda kinyume, mchafu na mpotofu.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 85-86
  • Imechapishwa: 08/06/2022