29. Hivi ndivo wanavoamini Khawaarij

Khawaarij. Ni wenye kutoka katika dini, wanaiacha dini, wanajitenga kutokamana na Uislamu, wanaenda kinyume na Mkusanyiko, wamepotea kutokamana na njia ya uongofu, wamemfanyia uasi mtawala na viongozi, wamewachomolea Ummah upanga, wamehalalisha damu na mali zao na wamewakufurisha wale wenye kupingana nao. Hakuna wanaosalimishwa isipokuwa wale wenye kuona vile wanavoonelea wao na wakaishi katika makazi ya upotofu wao.

Wanawatukana Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakwe na wale aliooa kwao, wanajitenga mbali nao na wanawatuhumu ukafiri na kashfa na wanaona kutofautiana nao katika mambo ya kidini.

Hawaamini adhabu ya kaburi, Hodhi na Uombezi. Wanaona kuwa mtu akishaingia Motoni basi hatoki kabisa. Wanaona kuwa yule ambaye atasema uwongo siku moja, akatenda dhambi ndogo au dhambi kubwa ambapo akafa pasi na kutubia, basi huyo ni kafiri  na atadumishwa Motoni milele. Wana ´Aqiydah moja kama Bakriyyah inapokuja katika nafaka na shilingi.

Sambamba na hilo wao ni Qadariyyah, Jahmiyyah, Murji-ah na Raafidhwah. Hawaoni kuswali isipokuwa nyuma ya maimamu wao tu. Wanaona kufaa kuchelewesha swalah kutoka nje ya nyakati zake. Wanaona kufaa kufunga kabla ya kuona mwezi mwandamo, na wanaona kufaa kufungua kabla ya kuona mwezi mwandamo. Wanajuzisha kufunga pasi na walii wala mamlaka, na wanaona kufaa kwa ndoa ya Mut´ah katika dini yao. Wanaona kufaa kuuza dirhamu moja kwa dirhamu mbili, mkono kwa mkono. Hawaoni kufaa kuswali ndani ya soksi za ngozi wala kupunguza juu yake.

Hawaoni kumtii mtawala. Hawaoni kuhitaji kujiunga na ukhaliyfah wa Quraysh. Wana mambo mengine mengi ambayo wanatofautiana na Uislamu na waislamu. Inatosha maoni, ´Aqiydah na dini yao ni namna hii ili kuthibitisha upotofu wao. Hawana lolote kuhusiana na Uislamu. Ni wenye kutoka [katika dini].

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 86-90
  • Imechapishwa: 08/06/2022