30. Baadhi ya mapote ya Khawaarij

Miongoni mwa majina ya Khawaarij ni pamoja na:

Haruuriyyah. Ni watu wenye kutoka Haruura´.

Azaariqah. Ni wafuasi wa Naafiy´ bin al-Azraq. Maoni yao ni mabaya zaidi na yaliyo mbali zaidi na Uislamu na Sunnah.

Najdiyyah. Ni wafuasi wa Najdah bin ´Aamir al-Haruuriy.

Ibaadhiyyah. Ni wafuasi wa ´Abdullaah bin Ibaadhw.

Swufriyyah. Ni wafuasi wa Daawuud bin an-Nu´maan wakati alipoambiwa:

“Hakika wewe ni mtupu (صفر) wa elimu.”

Bayhasiyyah, Maymuuniyyah na Khaazimiyyah.

Wote hawa ni Khawaarij, watenda madhambi mazito, wanaoenda kinyume na Sunnah, wenye kutoka nje ya dini, wazushi na wapotofu. Isitoshe ni wezi na majambazi.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 90-94
  • Imechapishwa: 08/06/2022