Swali: Ni ipi hukumu ya kusema “Swadaqah Allaahu al-´Adhwiym” baada ya kumaliza kusoma Qur-aan?
Jibu: Kusema “Swadaqah Allaahu al-´Adhwiym” baada ya kumaliza kusoma Qur-aan ni Bid´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), makhaliyfah waongofu, Maswahabah wengine na maimamu wa Salaf (Rahimahumu Allaah) wote hawakufanya hivo pamoja na kuwa wao walikuwa wakisoma sana Qur-aan, kuitilia umuhimu na kuijua zaidi. Hivyo kusema hivo na kulazimiana nalo baada ya kila kisomo ni Bid´ah iliyozuliwa. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:
“Atakayezusha katika dini yetu yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”
“Atakayefanya kitendo kisichokuwemo katika dini yetu atarudishiwa mwenyewe.”
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (118/04)
- Imechapishwa: 22/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)