Swali: Ni ipi hukumu ya kusema “Swadaqah Allaahu al-´Adhwiym” baada ya kumaliza kusoma Qur-aan?

Jibu: Kusema “Swadaqah Allaahu al-´Adhwiym” baada ya kumaliza kusoma Qur-aan ni Bid´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), makhaliyfah waongofu, Maswahabah wengine na maimamu wa Salaf (Rahimahumu Allaah) wote hawakufanya hivo pamoja na kuwa wao walikuwa wakisoma sana Qur-aan, kuitilia umuhimu na kuijua zaidi. Hivyo kusema hivo na kulazimiana nalo baada ya kila kisomo ni Bid´ah iliyozuliwa. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Atakayezusha katika dini yetu yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”

“Atakayefanya kitendo kisichokuwemo katika dini yetu atarudishiwa mwenyewe.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (118/04)
  • Imechapishwa: 22/08/2020