Inajuzu kusoma Qur-aan nyakati swalah imekatazwa?

Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma Qur-aan katika nyakati zilizotajwa kwenye Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Amekataza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuswali swalah ya sunnah wakati jua linapochomoza na wakati linapozama.

Jibu: Kusoma Qur-aan katika nyakati ambazo zimetajwa kwenye swali inajuzu kwa kukosekana dalili yenye kukataza. Asli ni kujuzu kusoma kutokana na Shari´ah kusisitiza hilo mpaka kuthibiti dalili yenye kukataza.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (4/110)
  • Imechapishwa: 22/08/2020