Kusoma Qur-aan kwa kuegemea, kusimama na kutembea

Swali: Je, inajuzu kusoma Qur-aan tukufu kwa ambaye anaegemea, amesimama au anatembea?

Jibu: Inajuzu kufanya hivo. Asli ni kujuzu. Hakukuthibiti dalili yenye kukataza. Allaah (Ta´ala) amesema akiwasifu werevu:

الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ

“Ambao wanamdhukuru Allaah kwa kusimama, na kwa kukaa na kwa kulala ubavuni mwao.” (03:191)

Kusoma Qur-aan ni miongoni mwa Dhikr.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (4/106)
  • Imechapishwa: 22/08/2020