Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
5 – Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:
“Watu waliona mwezi mwandamo. Nikamweleza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba nimeuona ambapo akafunga na akawaamrisha watu kufunga.”[1]
Ameipokea Abu Daawuud. Ameisahihisha Ibn Hibbaan na al-Haakim.
5 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba kuna mbedui mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akasema:
“Mimi nimeuona mwezi mwandamo. Akasema: “Wewe unashuhudia ya kwamba hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah?” Akasema: “Ndio.” Akasema: “Ndio.” Akamuuliza tena: “Unashuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ndio.” Ndipo akasema: “Ee Bilaal! Watangazie watu wafunge kesho!”[2]
Wameipokea watano na akaisahihisha Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan. an-Nasaa´iy ameonelea kuwa kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi[3].
Hadiyth ni dalili kwamba inatosha mtu mmoja kuripoti kuona mwezi mwandamo wa Ramadhaan. Ni mamoja awe mwanamume au mwanamke muda wa kuwa ni muislamu. Hayo ndio maoni ya ´Umar, ´Aliy na Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhum). Vilevile ndio maoni ya Ibn-ul-Mubaarak. Pia ndio maoni yaliyotangaa kutoka kwa Imaam Ahmad na sahihi kutoka kwa ash.Shaafi’iy.
Maoni ya pili yanasema kwamba si sahihi isipokuwa wawili. Hayo ndio maoni ya ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh). Imaam Maalik, al-Layth, al-Awzaa’iy na Ishaaq. Wanajengea hoja kwa Hadiyth ya ´Abdur-Rahmaan bin Zayd bin al-Khattwaab ambaye aliwatolea watu Khutbah katika siku ambayo wana shaka nayo:
”Nilikaa na Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwauliza ambapo wakanieleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Fungeni kwa kuonekana kwake fungueni kwa kuonekana kwake na tekelezeni ´ibaadah kwa ajili yake. Mkifunikwa na mawingu basi kamilisheni thelathini. Ikiwa mashahidi wawili watashuhudia, basi fungeni na fungueni.”
Wamesema kuwa muktadha wake inafahamisha kwamba haitoshi mtu mmoja. Isitoshe ushuhuda huu wa kuonekana mwezi mwandamo ni kufunga na kwa hiyo inafanana na ushahidi wa mwezi mwandamo wa kaunza Shawwaal. Maoni ya kwanza ni yenye nguvu zaidi. Kwa sababu Hadiyth ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ni dalili ya wazi. Kwa hivyo inapaswa kuifanyia kazi yale inayopelekea. Kuhusu dalili yao ni kwa njia ya muktadha. Lakini Hadiyth ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ni mashuhuri zaidi na ina dalili ya moja kwa moja. Kwa hivyo inapaswa kupewa kipaumbele. Kuhusu kipimo, kuna tofauti. Kwa sababu mwezi mwandamo wa Shawwaal inahusiana na kutoka kwenye ´ibaadah, wakati mwezi mwandamo wa Ramadhaan inahusiana na kuingia ndani ya ´ibaadah na hivyo kinachotakiwa ni kuchukua tahadhari. Na miongoni mwa kuchukua tahadhari ni kukubali ushahidi wa mtu mmoja.
Kuhusu kutoka kwenye swawm, haikubaliwia isipokuwa ushahidi wa watu wawili waadilifu kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi, kwa sababu ya ushahidi wa Hadiyth ya ´Abdur-Rahmaan bin Zayd.
Maoni ya pili yanasema kuwa inatosha kauli ya mtu mmoja, kwa sababu ni sehemu ya mwezi wa Ramadhaan na hivyo inafanana na sehemu ya kwanza. Haya ni maoni ya Abuth-Thawr, Ibn-ul-Munthir, Ibn Hazm na al-Khattwaabiy ameinukuu kutoka kwa baadhi ya Ahl-ul-Hadith[4]. as-Swan’aaniy[5] ameegemea kwayo na ikachaguliwa na ash-Shawkaaniy[6].
[1] Abu Daawuud (2342), Ibn Hibbaan (3447) na al-Haakim (1/423).
[2] Abu Daawuud (2340), at-Tirmidhiy (691), an-Nasaa’iy (2112), Ibn Maajah (1652), Ibn Khuzaymah (1923), Ibn Hibbaan (3446) na ad-Daarimiy (1692). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (907).
[3] as-Sunan al-Kubraa (3/99).
[4] Ma´alim-us-Sunan (03/226), “al-Muhallaa” (06/235) na “al-Mughniy” (04/419).
[5] Sub-us-Salaam (04/112).
[6] Nayl-ul-Awtwaar (04/210-211).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/14-17)
- Imechapishwa: 30/01/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/14-17)
Imechapishwa: 30/01/2025
https://firqatunnajia.com/11-hadiyth-watu-waliona-mwezi-mwandamo/