Swali: Ni ipi hukumu ya Sunnah ya Fajr akiamka muislamu kuswali baada ya kuchomoza kwa Fajr? Je, imependekezwa kuitekeleza au ni lazima kwake papo hapo kuswali swalah ya Fajr kisha ndio aswali Sunnah yake?
Jibu: Sunnah kwa muumini atangulize Sunnah ya Fajr ambayo anatakiwa kuiswali nyumbani kisha atoke kwenda msikitini. Akifika na haijaanza, basi ataswali Rak´ah mbili za mamkuzi ya msikiti. Hii ndio Sunnah. Akiwa nyumbani hakuswali bali amekuja msikitini, basi ataswali Sunnah ya Raatibah msikitini Rak´ah mbili itayomtosheleza kutokamana na swalah ya mamkuzi ya msikiti. Ni sawa endapo atanuia zote mbili. Nakusudia Sunnah ya Fajr na swalah ya mamkuzi ya msikiti.
Lakini ikiwa Sunnah hii itampita kwa mfano kwa yeye kupitiwa na usingizi na asiamke isipokuwa baada ya kuchomoza kwa Fajr, basi ataanza Sunnah ya Fajr kisha aswali faradhi. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yeye na Maswahabah zake katika baadhi ya safari kutokamana na swalah ya Fajr.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/377)
- Imechapishwa: 09/11/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Aanze na swalah ya Fajr au Sunnah yake?
Swali: Ni ipi hukumu ya Sunnah ya Fajr pindi muislamu anapoamka kuswali baada kuchomoza kwa jua? Je, inapendeza kwake kuiswali au ni lazima kwake papohapo kuanza na swalah ya Fajr kasha ndio aswali Sunnah yake? Jibu: Sunnah kwa muumini ni yeye kutanguliza Sunnah ya Fajr kwa njia ya kwamba aiswali…
In "Tahiyyat-ul-Masjid - Swalah ya mamkuzi ya msikiti"
52. Makatazo ya kuswali Sunnah baada ya kukimiwa swalah ya faradhi
Swali 52: Tunawaona baadhi ya watu wanapoingia msikitini kwa ajili ya kuswali Fajr na kumeshakimiwa kwa ajili ya swalah wanaswali Rak´ah mbili za Fajr kisha wanajiunga na imamu. Ni ipi hukumu ya hilo? Bora ni wao kuziswali moja kwa moja baada ya Fajr au wasubiri kuchomoza kwa jua? Jibu: Haijuzu…
In "3. Swalah ya mkusanyiko, uimamu na kumfuata imamu"
Anaswali Sunnah baada ya kukimiwa swalah
Swali: Tunaona baadhi ya watu wanapoingia msikitini kwa ajili ya kuswali Fajr na kumeshakimiwa swalah basi wanaswali Rak´ah mbili za Fajr kisha baadaye wanajiunga na imamu. Ni ipi hukumu ya hilo? Je, bora mtu aiswali moja kwa moja baada ya Fajr au asubiri mpaka lichomoke jua? Jibu: Haijuzu kwa ambaye…
In "Rawaatib na Nawaafil"