52. Makatazo ya kuswali Sunnah baada ya kukimiwa swalah ya faradhi

Swali 52: Tunawaona baadhi ya watu wanapoingia msikitini kwa ajili ya kuswali Fajr na kumeshakimiwa kwa ajili ya swalah wanaswali Rak´ah mbili za Fajr kisha wanajiunga na imamu. Ni ipi hukumu ya hilo? Bora ni wao kuziswali moja kwa moja baada ya Fajr au wasubiri kuchomoza kwa jua?

Jibu: Haijuzu kwa ambaye ameingia msikitini na kumeshakimiwa swalah akaswali Raatibah au swalah ya mamkuzi ya msikiti. Bali ni lazima kwake kuingia pamoja na imamu katika swalah ya sasa. Mtume (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam):

“Kunapokimiwa swalah basi hakuna swalah nyingine isipokuwa ile ya faradhi.”

Ameipokea Imaam Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Hadiyth hii inaenea swalah ya Fajr na nyinginezo.

Baada ya hapo ana khiyari; akitaka ataswali Raatibah baada ya swalah na akitaka pia anaweza kuichelewesha mpaka kuchomoza kwa jua, na ndio bora zaidi. Imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) yanayofahamisha yote mawili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 57-58
  • Imechapishwa: 06/09/2022