Swali 53: Kuna mtu ametuswalisha na akatoa Tasliym moja upande wa kuliani. Je, inafaa kufupilizika katika moja? Je, imepokelewa katika Sunnah kitu katika hayo?

Jibu: Wanazuoni wengi wameonelea kwamba Tasliym moja inatosha. Kwa sababu imepokelewa katika baadhi ya Hadiyth yanayofahamisha juu ya hilo[1]. Jopo la wanazuoni wengine wameona kwamba ni lazima kutoa Tasliym mbili kwa sababu ya kuthibiti Hadiyth nyingi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya hilo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

Maoni haya ya pili ndio ya sawa.

Maoni yanayosema kwa kukata kufaa kwa Tasliym moja ni dhaifu kutokana na unyonge wa Hadiyth zilizopokelewa juu ya hilo na kutosema wazi kinachotakikana. Endapo zingelikuwa zimesihi basi zingelikuwa ni Shaadhah kwa sababu zitakuwa zimekwenda kinyume na yaliyo Swahiyh, thabiti na wazi zaidi. Lakini ambaye atafanya hivo kwa ujinga au kwa kuamini kuwa Hadiyth juu ya jambo hilo zimesihi, basi swalah yake ni sahihi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/108-tasliym/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 58
  • Imechapishwa: 06/09/2022