54. Hesabu iliyozidishwa na imamu kwa ambaye amekuja kuchelewa

Swali 54: Ambaye amekuja kuchelewa akijiunga na imamu akaswali pamoja naye kisha ikambainikia kuwa imamu ameswali Rak´ah tano – je, ahesabu hiyo Rak´ah iliyoongezwa aliyoiswali pamoja na imamu kwa njia ya kwamba aswali Rak´ah mbili peke yake au asiizingatie na badala yake aswali Rak´ah tatu?

Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba hatoihesabu. Kwa sababu haina malengo katika hukumu ya ki-Shari´ah. Kilicho cha lazima ni kutomfuata imamu kwa ambaye atatambua kuwa imezidishwa. Ni lazima kwa ambaye amekuja amechelewa asiifuate. Huyu mkusudiwa analazimika kulipa Rak´ah tatu kwa sababu ukweli wa mambo ni kwamba hakuwahi isipokuwa Rak´ah moja peke yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 59
  • Imechapishwa: 06/09/2022