Atakayeamka baada ya kuchomoza alfajiri ataanza Sunnah ya Fajr au faradhi kwanza?

Swali: Ni ipi hukumu ya Sunnah ya Fajr akiamka muislamu kuswali baada ya kuchomoza kwa Fajr? Je, imependekezwa kuitekeleza au ni lazima kwake papo hapo kuswali swalah ya Fajr kisha ndio aswali Sunnah yake?

Jibu: Sunnah kwa muumini atangulize Sunnah ya Fajr ambayo anatakiwa kuiswali nyumbani kisha atoke kwenda msikitini. Akifika na haijaanza, basi ataswali Rak´ah mbili za mamkuzi ya msikiti. Hii ndio Sunnah. Akiwa nyumbani hakuswali bali amekuja msikitini, basi ataswali Sunnah ya Raatibah msikitini Rak´ah mbili itayomtosheleza kutokamana na swalah ya mamkuzi ya msikiti. Ni sawa endapo atanuia zote mbili. Nakusudia Sunnah ya Fajr na swalah ya mamkuzi ya msikiti.

Lakini ikiwa Sunnah hii itampita kwa mfano kwa yeye kupitiwa na usingizi na asiamke isipokuwa baada ya kuchomoza kwa Fajr, basi ataanza Sunnah ya Fajr kisha aswali faradhi. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yeye na Maswahabah zake katika baadhi ya safari kutokamana na swalah ya Fajr.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/377)
  • Imechapishwa: 09/11/2021