Asiyekuwa msomi kumkufurisha mwenye kutumbukia katika shirki

Swali: Wengi wanaojinasibisha na Salafiyyah wanashurutisha kwamba wanachuoni peke yao ndio wasimamishe hoja. Pindi asiyekuwa msomi anapotumbukia katika shirki wanakataza mtu asimkufurishe.

Jibu: Kusimamisha hoja ni kule kumbainishia dalili. Huku ndio kusimamisha hoja. Kila mmoja na kiasi cha uwezo wake.

Swali: Je, ni wajibu kwa asiyekuwa msomi amkufurishe mwenye kutumbukia katika kufuru?

Jibu: Ikimthibitikia kuwa amefanya kufuru amekufuru. Kipingamizi kiko wapi? Ikimthibitikia yenye kuwajibisha kufuru amkufurishe. Kwa mfano anayekataa kumkufurisha Abu Jahl, Abu Twaalib na ´Utaybah bin Rabiy´. Huyo ameshasimamikiwa na dalili ya kwamba hawa wamekufa juu ya kufuru na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawapiga vita makafiri siku ya Badr.

Swali: Je, wasiokuwa wasomi wakatazwe kukufurisha?

Jibu: Asiyekuwa msomi asikufurishe isipokuwa kwa dalili. Asiyekuwa msomi hana elimu. Isipokuwa ikiwa kama ana elimu kidogo juu ya mambo maalum. Kwa mfano anayepinga uharamu wa zinaa. Mtu kama huyu anakufuru kwa ambaye si msomi na msomi. Kwa sababu hakuna utata na hakuhitajiki dalili. Hivi ndivyo ninavyosema. Mfano mwingine kama anasema inajuzu kwa watu kumuabudu asiyekuwa Allaah. Je, kuna yeyote mwenye shaka juu ya hili? Hakuhitajiki dalili. Kwa mfano akasema kuwa inajuzu kwa watu kuyaabudu masanamu, nyota, majini au akasema kuwa swalah sio wajibu na anayetaka, anaswali, asiyetaka, aache, mwenye kusema haya anakufuru. Akomeke katika mambo yenye kutatiza ambayo yanaweza kuwa ni yenye kufichikana kwa ambaye si msomi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 34
  • Imechapishwa: 12/11/2016