Swali: Je, Mtume (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam) amekingwa na kukosea? Vipi tutajumuisha kati ya kukingwa kwa Mtume (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam) na Kauli ya Allaah (Ta´ala):

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ

”Alikunja kipaji na akageuka.”? (80:01)

Jibu: Mtume (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam) amekingwa na shirki, madhambi makubwa na kukosea kwa yale anayofikisha kutoka kwa Allaah. Ama kuhusiana na madhambi madogo hapana [hakukingwa]. Allaah (Ta´ala) Amesema:

لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ

“Ili Allaah Akusamehe yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayokuja.” (48:02)

وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ

“Na omba msamaha kwa dhambi zako na (kwa dhambi za) Waumini wa kiume.” (47:19)

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ

”Alikunja kipaji na akageuka.”? (80:01)

Vilevile inawezekana ikawa ni kwenda kinyume na lililo la aula. Lakini kutokamana na kwamba hadhi yake ni ya juu (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam) ndio Allaah akawa Amemuadhibu…

Kisa hichi [´Abasa] Allaah Amekiteremsha kumlaumu Mtume Wake mtukufu kwa kuwa amefanya lililo kinyume na la aula. Kama tulivyotangulia kusema, Mtume (Swalla Allaah ´alayhi wa sallam) amekingwa na shirki, madhambi makubwa na amekingwa vilevile na kukosea kwa yale anayofikisha kutoka kwa Allaah. Ama baadhi ya madhambi madogo na kwenda kinyume na la aula, yanamtokea lakini hata hivyo Amesamehewa kama mmevyosikia. Hili ni kutokana na andiko la Qur-aan:

لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ

“Ili Allaah Akusamehe yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayokuja.” (48:02)

لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ

“Ili Allaah Akusamehe yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayokuja.” (48:02)

وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ

“Na omba msamaha kwa dhambi zako na (kwa dhambi za) Waumini wa kiume.” (47:19)

Vilevile inawezekana kuwa sio maasi bali ni kwenda kinyume na lililo la aula. Lakini ilivokuwa hadhi yake ni ya juu ndio Allaah akawa Amemlaumu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4738
  • Imechapishwa: 17/11/2014