Namna hii ndivyo zinakuwa hali za wengi wanaohudhuria kwenye maulidi

Miongoni mwa [maovu yanayotokea katika maulidi] ni wanaume na wanawake kuchanganyika.

Isitoshe wengi wanaohudhuria katika maulidi hali zao zinakuwa mbaya. Wengi wao hawaswali. Hawahifadhi swalah. Wanafanya mambo ya maovu. Wanapupia Bid´ah na wanaacha mambo ya wajibu. Lililo la wajibu kwa muislamu ni kufuata na aache kuzusha. Lau ingelikuwa ni kheri wangelitutangulia nalo Maswahabah na Taabi´uun. Vilevile lau yangelikuwa ni kheri basi Allaah Angelituwekea nayo [katika Shari´ah]. Kwa haya tunapata kubainikiwa kuwa maulidi ni katika Bid´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4738
  • Imechapishwa: 17/11/2014