Swali: Vipi kuhusu kauli “Jum´ah mubaarakah”?

Jibu: Neno hili “Jum´ah mubaarakah” halina asli. Kupeana hongera kwa ajili ya Ijumaa ni jambo lisilokuwa na asli. Kupeana hongera inakuwa siku ya ´Iyd-ul-Fitwr na ´Iyd-ul-Adhwhaa. Ama kuhusu siku ya Ijumaa hapana.

Vilevile kuhusiana na mwanzoni wa kuingia mwaka mpya [wa Kiislamu] ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah kupeana hongera kwa kuingia kwa mwaka wa Hijriyyah. Haya yote hayakuwekwa katika Shari´ah, bali ni katika Bid´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4745
  • Imechapishwa: 01/05/2015